Thursday , 27th Oct , 2016

Kocha wa Manchester United, Jose Mourinho ameshitakiwa na Chama Cha Soka nchini Uingereza FA, juu ya maneno yake kwa mwamuzi, Anthony Taylor, aliyechezesha mechi baina ya Manchester United na Liverpool wiki mbili zilizopita.

Jose Mourinho

 

Mourinho, alisema mwamuzi Taylor, anayekaa karibu na Uwanja wa Old Trafford, anaweza kuwa na wakati mgumu kuchezesha mechi za mahasimu hao, baada ya mashabiki wengi wa Liverpool, kutokuwa na imani naye.

Taarifa ya FA imesema maneno hayo ya Mourinho yanaweza kuleta uchochezi na hivyo, amevunja kanuni na taratibu za FA.

FA, imempa Mreno huyo, hadi Oktoba, 31 Jumatatu ijayo, saa 2, usiku kwa saa za Afrika Mashariki awe amejibu mashtaka yanayomkabili, na akipatikana na makosa anaweza kupigwa faini.