Saturday , 7th May , 2016

Mchezaji wa klabu ya Dinamo Bucharest ambaye pia ni kiungo wa Cameroon, Patrick Ekeng, amefariki dunia kwa shambulio la moyo baada ya kuanguka uwanjani akicheza mpira.

Ekeng alianguka uwanjani katika dakika ya 70 ya mchezo wa ligi uliokuwa ukionyeshwa na televisheni ya Romania, baina ya Dinamo na Viitorul.

Ilikuja elezwa baadaye kuwa Ekeng amefariki dunia hospitalini saa mbili kupita tangu akimbizwe kutoka uwanjani.

Kufuatia tukio hilo Shirikisho la Soko la Romania, limetangaza kusitisha michezo yote ya ligi ya nchi hiyo ya mwishoni mwa wiki hii.