
Boniface Pawasa (kushoto) na Mbwana Samatta na John Bocco.
''Mimi naamini nia ipo na uwezo tunao wa kuwafunga nyumbani kwao Lesotho na wachezaji wajue tu mchezo umeshaanza walipopanda ndege hapa kwenda kuweka kambi nchini Afrika Kusini'', amesema mchezaji huyo wa zamani wa Simba.
Amewataka wachezaji kutojiamini kupita kiasi bali wawe na imani pamoja na mtazamo wa kushinda ambao utawajenga zaidi kiushindani na mwisho wakapate matokeo mazuri ugenini jambo ambalo linawezekana.
Aidha Pawasa amewakumbusha Watanzania kuwa wanatakiwa kuwapa nguvu wachezaji huku akieleza kufurahishwa na uzalendo wa mashabiki ambao wamejitolea kusafiri kwa basi kuelekea Lesotho.
Amemaliza kwa kusema kuwa kikosi cha Taifa Stars chini ya kocha Emmanuel Amunike kina uwezo wa kufanya lolote kwenye mpira hivyo wachezaji wanatakiwa kutumia kila nafasi wanayoipata.