
Beki wa Real Madrid Marcelo (kulia)akijaribu kupandisha mashambulizi .
Kocha zinedine Zidane alikiwa na kikosi kilichokuwa na upungufu wa Karim Benzema na Gareth Bale akimuanzisha Cristiano Ronaldo ambaye ndiye aliyeifungia bao Madrid dakika 33.
Dakika mbili baadaye Madrid wakapata penati ambayo Cristinao Ronaldo akaipoteza baada ya kuokolewa na kipa wa Malaga Carlos Idriss Kameni.
Dakika ya 66 Raul Albentosa aliisawazishia Malaga akimalizia pasi nzuri ya beki wa kati Welington na kuufanya mchezo umalizike kwa matokeo ya sare ya bao 1-1 hadi mwisho wa mchezo.
Hii inakuwa penati ya saba kwa Ronaldo kukosa msimu huu ikiwa ni idadi sawa na mpinzani wake Lionel Messi.
Katika hatua nyingine Atletico Madrid wameisafishia njia Barcelona kutawala kileleni mwa ligi hiyo baada ya hapo jana kutoka sare tasa na Villareal.
Barcelona inaongoza ligi ikijivunia alama 63 huku Atletico Madrid ikifuatia kwa alama zake 55 nayo Real Madrid ikikamata nafasi ya tatu kwa alama 54.
MATOKEO
Celta de Vigo 3 SD Eibar 2
Rayo Vallecano 2 Sevilla 2
Athletic de Bilbao 0 Real Sociedad 1
Granada CF 1 Valencia 2