
Wachezaji wa Taifa Stars
''Maandalizi yanaendelea vizuri wachezaji wa kimataifa wanaendelea kuwasili lakini kikubwa tu wachezaji waliokuwa majeruhi Beno Kakolanya na Yahya Zayd wamerejea kwenye hali zao nzuri na wanaendelea na programu za mwalimu'', amesema.
Ndimbo pia amewataja wachezaji wa kimataifa waliowasili ni mabeki Abdi Banda wa Baroka FC ya Afrika Kusini, Hassan Kessy wa Nkana FC ya Zambia na washambuliaji Rashid Mandawa wa BDF XI ya Botswana na Thomas Ulimwengu aliyevunja mkataba na El Hilal ya Sudan.
Wengine ni kiungo wa Petrojet ya Misri, Himid Mao ambaye anawasili Afrika Kusini leo, wakati kesho kiungo mshambuliaji, Simon Msuva wa Difaa Hassan El-Jadidi ya Morocco atajiunga pia na kambi hiyo.
Taifa Stars itaondoka mjini Bloemfontein, Afrika Kusini Ijumaa kwenda Maseru kwa basi kwa ajili ya mchezo wa Kundi L kufuzu Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON) mwakani nchini Cameroon dhidi ya wenyeji, Lesotho Jumapili.