Sunday , 27th Aug , 2017

Timu ya Young Africans tayari imeshaweka wazi risasi zake za mashambulizi dhidi ya Lipuli FC zikiongozwa na Mkongomani Papy Tshishimbi katika mchezo unaotarajia kuchezwa leo saa kumi jioni katika uwanja wa Uhuru jijini Dar es saalam.

Mechi hii ya ufunguzi wa ligi unatazamwa kwa shauhuku kubwa na mashabiki wa timu hiyo baada ya Jumatano iliyopita kukubali kichapo cha mkwaju kutoka kwa watani zao Simba SC.

Kupitia ukurasa wao wa mtandao wa Instagram Yanga wamekiweka kikosi kitakachopambana leo.

"Yanga SC burudani ya soka iko uwanja wa Uhuru leo, mabingwa mara27 wako uwanjani dhidi ya Lipuli Fc" imeandikwa katika taarifa hiyo.