Monday , 27th Oct , 2014

Chama cha Judo nchini JATA kinatarajia kutoa semina ya waamuzi wa mchezo huo inayotarajiwa kufanyika Novemba 7 mwaka huu jijini Dar es salaam.

Akizungumza na East Africa Radio, Katibu wa JATA, Innocent Malya amesema mafunzo hayo yenye lengo la kupata waamuzi bora watakaosimamia michuano ya Judo Klabu Bingwa Taifa pamoja na yale ya kanda ya Tano yatahusisha waamuzi kutoka mikoam mbalimbali nchini ambao ni wanachama wa chama hicho.

Malya amesema baada ya mafunzo hayo, wanatarajia kutafuta timu za vijana ambazo zitaweza kushiriki mashindano mbalimbali na kuweza kuitangaza nchi katika mchezo huo.

Tags: