Monday , 24th Mar , 2014

Uongozi wa klabu ya soka ya Simba umesema kuwa bado haujakata tamaa yakuwania nafasi mbili za juu katika ligi kuu ya soka Tanzania bara japo timu hiyo bado iko nyuma kwa pointi 11 dhidi ya vinara wa ligi hiyo Azam fc

Afisa habari wa timu hiyo Asha Muhaji amesema kuwa matokeo wanayopata hivi sasa ni sehemu ya mchezo na timu inapofanya makosa basi nyingine hutumia nafasi hiyo kupata matokeo

Aidha Asha ameongeza kuwa pamoja na kubakiza michezo minne na timu nyingine za juu yao zikiwa na mechi za viporo hilo haliwakatishi tamaa kwani hata wao wanaweza kuteleza na wao wakashinda michezo yao na kushika moja ya nafasi mbili za juu.