
Mlinda Mlango wa zamani, Peter Manyika
Manyika amesema, mara baada ya Chad kujitoa katika kuwania Afcon malengo ya baadhi ya timu katika kundi G zilizopo timu za Nigeria, Misri na Tanzania yamevurugika ingawa mechi bado hazijaisha.
Manyika amesema, unafuu upo kwa Misri mwenye pointi nne ambaye anacheza kesho dhidi ya Nigeria na iwapo akishinda atakuwa na pinti saba huku wakiwa wamebakiwa na mechi moja ya marudiano dhidi ya Tanzania itakayopigwa Juni jijini Dar es salaam huku na Nigeria pia yenye pointi mbili ikiwa imebakiwa na mechi moja ya marudiano dhidi ya Tanzania pia itakayopigwa nchini Nigeria.
Manyika amesema, iwapo katika mchezo wa kesho dhidi ya Misri na Nigeria utakuwa sare itakuwa na unafuu ili Stars kujiandaa zaidi ili kupambana kuweza kusonga mbele.
Taifa Stars ilichapwa bao 3-0 na Misri katika mchezo wa awali uliopigwa nchini Misri hapo Juni 13 mwaka jana ambapo katika mchezo dhidi ya Nigeria uliopigwa Septemba tano mwaka jana Uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam timu hizo ziliweza kutoshana nguvu kwa kutoa sare ya bila kufungana.