Kikosi ya Yanga SC kikiwa katika mazoezi kujiandaa kuwavaa Mbao Fc
Mwalimu huyo amesema hawezi kuidharau Mbao FC kwani ni timu nzuri na yenye ushindani mkubwa hivyo wanahitaji kucheza kwa tahadhari na umakini mkubwa ili kuibuka na ushindi wa pointi zote tatu.
"Tumejiandaa vyema na tunamshukuru Mungu tumemaliza mazoezi yetu salama na tupo tayari sasa kuwavaa Mbao Fc, kikubwa mashabiki wetu wa Mwanza na mikoa ya karibu wafike kwa wingi waje kuona mpira safi kabisa toka kwa vijana wao na tunaamini ata Mbao nao wataonyesha mpira mzuri na waupinzani mkubwa"-Juma Mwamusi Mwalimu Yanga SC.
Aidha, katika mchezo huu wa nusu fainali ya Kombe la FA utakaochezwa leo saa kumi jioni katika viwanja vya CCM Karumba, Jijini Mwanza mshindi wake atakutana kwenye fainali na Simba SC iliyoshinda goli 1:0 dhidi ya Azam FC jana.








