Tuesday , 11th Oct , 2016

Chama Cha Waandishi wa Habari za Michezo Tanzania (TASWA), kimeandaa kongamano maalum Oktoba 20 mwaka huu kuzungumzia kuhusiana na mifumo ya kiuendeshaji ambayo klabu kongwe nchini za Simba na Yanga zipo mbioni kuingia.

Katibu Mkuu wa TASWA, Amir Mhando

Katibu Mkuu wa TASWA, Amir Mhando amesema kwamba kongamano hilo linatokana na klabu za Simba na Yanga, hivi sasa katika mchakato wa kubadilisha mfumo wao wa kiundeshaji.

Amesema Simba inataka kuingia utaratibu wa hisa, wakati Yanga inataka kukodishwa, huku, TASWA inaamini yapo mambo ambayo pengine wanachama, mashabiki na hata wadau wa mpira wa miguu na wanamichezo kwa ujumla wanapaswa kufahamu kwa undani zaidi kuhusiana na mifumo hiyo miwili ili kuwe na uelewa mpana zaidi.