Wednesday , 12th Oct , 2016

Shirikisho la Mpira wa Kikapu Tanzania TBF limesema limejifunza mambo mengi kupitia mashindano ya kimataifa ya klabu bingwa ya mpira wa kikapu Kanda ya Tano yaliyomalizika hivi karibuni na kushuhudiwa wageni wakitwaa ubingwa kwa wanaume na wanawake.

Uwanja wa Ndani wa Taifa Jijini Dar es Salaam.

Akizungumza na Hotmix Michezo Kamishna wa Ufundi wa TBF Manase Zabron amesema hivi sasa wanajipanga kuhakikisha wanafanya vyema katika michuano ijayo na kimsingi anakubali kabisa matokeo mabovu ya timu za Tanzania yalitokana na kuzidiwa kiufundi na wageni.

Manase amesema kufuatia matokeo hayo sasa shirikisho hilo hivi sasa limeona ni vyema kuwepo na mpango wa muda mrefu wa kukuza vijana kwa kuwapa mafunzo ya mchezo huo katika nyanja mbalimbali.

Aidha amesema moja ya mipango hiyo ama mikakati ya kuondokana na kuwa wasindikizaji katika michuano mbalimbali ya kimataifa ni kuandaa programu maalum kwa vijana ili kukuza mchezo huo.

Amesema akitolea mfano michuano ya Kanda ya Tano na kukiri kwamba timu za Tanzania zilizidiwa kiufundi pamoja na kujitahidi kupambana hadi dakika za mwisho.