
Afisa Habari wa Azam FC Jaffery Iddy Maganga amesema, timu 16 ni chache kwani Tanzania ni kubwa na kama kungekuwa na uwezekano kila mkoa ungekuwa na timu kwani kungekuwa na ligi ya ushindani mkubwa sana.
Maganga amesema, miundombinu ya nchi nayo inalazimisha kuwa na timu chache kwani suala zima la kusafiri pia linaleta tabu kwa timu.
Maganga amesema, katika soka timu zinatakiwa ziwe nyingi ili ushindani uwe mkubwa kwani itaepusha pia timu kujitangazia ubingwa huku ikiwa na mechi nne mkononi hivyo kutakapokuwa na timu nyingi itakuwa sio rahisi kwa timu kutangaza ubingwa mapema.
Kwa upande mwingine Maganga amesema, kuelekea msimu ujao wa Ligi Kuu ya Soka Tanzania bara vilabu vinatakiwa kutumia muda mzuri wa kujiandaa kabla ligi haijaanza na sio kusubiri ligi inaanza ndipo vinaanza maandalizi na matokeo yake timu inakuwa ya mwisho mapema kabla ligi haijaisha.