
Aishi amesema, wameshapita katika hatua ya awali hivyo wamejiandaa kwa ajili ya kuweza kupambana zaidi katika mchezo unaofuata ambao watakutana na Esperance ya nchini Tunisia na kuweza kuipeperusha bendera ya Taifa katika mashindano hayo.
Aishi amesema, walishajiandaa tangu hapo awali japo vilabu wanavyokutana navyo vimeshashiriki mashindano hayo mara nyingi lakini kwa kuwa walikuwa wanajua tangu mwanzo kuwa wanakutana na vilabu ambavyo vinawachezaji wazuri na wao kama wachezaji watajitahidi kujituma ili kuweza kufanya vizuri.
Azam FC inatarajia kukutana na Timu ya Esperance ya Nchini Tunisia kati ya Aprili nane au 10 katika raundi ya pili ya kombe la shirikisho Afrika baada ya kuitoa timu ya Bidvest ya nchini Afrika kusini kwa jumla ya bao 7-3.