Tuesday , 4th Nov , 2014

Michuano ya Kitaifa ya mchezo wa Judo inatarajiwa kuanza Novemba Saba mwaka huu jijini Dar es salaam kwa kushirikisha vilabu sita kati ya Nane vilivyoalikwa katika ushiriki wa mashindano hayo.

Akizungumza na East Africa Radio, Katibu wa Chama cha Judo nchini JATA, Innocent Malya amesema walialika vilabu mbalimbali kutoka mikoa ambayo ni wanachama wa JATA lakini vilabu Sita ndivyo vimehakiki ushiriki na vinaendelea na mazoezi ya mwisho kwa ajili ya michuano hiyo.

Malya amesema viongozi wa vilabu shiriki katika mashindano hayo wanatakiwa kuweka jitihada katika mazoezi ili kuweza kupata timu bora ya taifa ambayo itashiriki mashindano kanda ya Tano hapo mwakani huku Tanzania ikiwa nchi Mwenyeji wa michuano hiyo.