Kwa muda wa wiki tatu sasa Burundi imekuwa kwenye vurugu za kisiasa ambapo vyama vya upinzani, raia na taasisi za kidini nchini humo vimekuwa kwenye maandamano yasiyo na ukomo kupinga uamuzi wa Rais Pierre Nkurunziza kutaka kugombea urais kwa muhula wa tatu.
Shirikisho la mchezo huo barani Afrika limeanza kufanya mazungumzo na vyama vya nchi jirani za Kenya na Rwanda kuona uwezekano wa kuyahamisha kwenye moja ya nchi hizo.
Kwa upande wake, chama cha mchezo wa Judfo nchini Tanzania JATA, kimesema hakijui hatma ya ushiriki wake katika michuano hiyo kutokana na kuhofia hali ya kiusalama hivyo wanasikilizia iwapo kama nchi hizo za Kenya na Rwanda kama zimekubali uenyeji.