
Aliyekuwa Mlinda mlango wa Simba SC,Uganda na IBV Vestmanaeyjar ya Iceland, Marehemu Abel Dhaira
Manyika amesema, Dhaira alikuwa ni kipa aliyekuwa anastahili kucheza nje kutkana na kipaji chake na ndio maana hakukaa sana nchini mwake Uganda na Simba kwani timu zilikiona kipaji chake na kuweza kumchukua.
Dhaira amefariki hapo jana akiwa na umri wa miaka 28 na Januari mwaka huu ndiyo aligundulika kuwa na ugonjwa wa kansa ya utumbo.
Hadi mauti yanamkuta alikuwa bado ni kipa wa IBV Vestmanaeyjar ya Iceland.