Friday , 18th Jan , 2019

Shirikisho la soka nchini (TFF), kupitia kwa Bodi ya Ligi imeshusha rungu kwa waamuzi waliochezesha mchezo wa ligi kuu namba 124 kati ya JKT Tanzania dhidi ya Simba SC uliopigwa kwenye uwanja wa Mkwakwani Tanga.

Simba SC wakiwa kwenye mazoezi.

Akitangaza maamuzi ya Bodi ya ligi leo Januari 18, 2019, Mtendaji mkuu wa Bodi hiyo Boniface Wambura amesema kamati ya ligi imepitia mchezo mzima baada ya malalamiko ya JKT Tanzania kuhusu uchezeshaji wa waamuzi.

Mwamuzi msaidizi namba mbili katika mchezo huo, Mashaka Mwandembwa amefungiwa miezi mitatu kwa kushindwa kutafsiri sheria ya kuotea 'offside' huku mwamuzi wa kati Mabaka Rashid akipewa onyo kali.

Pia katika mechi namba 180 iliyohusisha Simba na Singida United kamati imewapiga faini ya shilingi laki mbili Singida United kwa kugoma kuingia kwenye vyumba vya kubadilishia nguo na badala yake wakatumia chumba cha waandishi wa habari.

Katika mchezo mwingine namba 167 uliokutanisha timu za Yanga na Ruvu Shooting umekuja na maamuzi ya Mtunza vifaa wa Ruvu Shooting Augustine Parangwa kufikishwa kwenye kamati ya nidhamu ya TFF kwa kutoa lugha ya matusi kwa waamuzi.

Zaidi msikilize Wambura akifafanua zaidi.