Tuesday , 18th Oct , 2016

Chama cha mchezo wa Karate, Tanzania, (TKA) , kimewataka walimu wa shule za msingi, Tanzania, kufika Ukumbi wa Utamaduni wa Urusi, ili kuandikisha vijana wao kwa ajili ya Mashindano ya Karate mwezi ujao.

Vijana katika mazoezi ya Karate

Mwenyekiti wa TKA Sensei Willy Ringo, kwa niaba ya Kamati ya Utendaji ya Chama hicho amesema lengo ni kutaka kukutana na kuona umuhimu wa kuendeleza vipaji vya watoto wa shule za msingi katika mchezo wa Karate.

Mashindano hayo, yanatarajiwa kufanyika kati ya Oktoba 25-28, na kwa kuanzia, Ringo amesema gharama za kuleta vijana hao, zitakuwa za wazazi husika na shule zao, lakini baada ya mashindano kutakuwa na vyeti, na zawadi mbali mbali, kutoka Chama Cha Karate nchini.