
Akizungumza jijini Dar es salaam, Meneja Masoko wa Kampuni ya Coca Cola, Morice Njowoka amesema, watoto mwengi wanashindwa kugaanya muda wao katika upande wa michezo na masomo ya darasani kutokana na kushindwa kutambua umuhimu wa michezo hapa nchini.
Kwa upande wake, mwanafunzi aliyeibuka mchezaji bora katika michuano ya Copa Cocacola ya vijana chini ya Umri wa miaka 15 mwaka jana, Ally Mabuyu amesema, wanafunzi hawatakiwi kukata tamaa katika michezo wkani kila mchezaji alianzia chini na baadaye akayafiki malengo.