
Mchezo wa JKU na Nyasa Big Bullets
Mchezo huo uliofanyika katika uwanja wa Amani, Big Bullets imetoka sare ya bila kufungana na JKU ambapo sasa imerejea Dar es salaam tayari kupambana na Simba.
Nyasa Big Bullets imekuja nchini kwaajili ya mchezo wa kirafiki dhidi ya Simba, utakaofanyika jioni ya leo katika uwanja wa taifa, ikiwa ni katika maandalizi ya michuano ya klabu bingwa Afrika na kombe la shirikisho itakayoanza baada ya mapumziko ya michezo ya kimataifa.
Katika michuano hiyo ya klabu bingwa Afrika, Big Bullets itapambana na Gor Mahia ya Kenya, Novemba 27 huku JKU ikitarajia kucheza na Al-Hilal ya nchini Sudan.
Mabingwa watetezi wa ligi kuu Tanzania bara Simba itapambana na Mbabane Swallows ya nchini Swartzland kati ya Novemba 27 na 28 kwenye uwanja wa taifa jijini Dar es salaam kabla ya marudiano, Disemba 4 na 5 mjini Mbabane.