Thursday , 24th Jan , 2019

Shirikisho la Soka Barani Afrika CAF limeiengua klabu ya Ismaily ya nchini Misri kwenye orodha ya timu za Kundi C Ligi ya Mabingwa barani humo.

Mshambuliaji, Yahya Zayd (kushoto) pamoja na wachezaji wa Ismaily (kulia) wakishangilia

Timu hiyo ya Ismailia anayochezea mshambuliaji chipukizi Mtanzania, Yahya Zayd imeenguliwa katika kundi lake kutokana na mashabiki wake kufanya vurugu mwishoni mwa mchezo wa hatua ya makundi dhidi ya Club Africain ya nchini Tunisia.

Mwamuzi wa mchezo huo, Neant Alioum alilazimika kusitisha mchezo dakika za mwisho kutokana na vurugu za mashabiki wa Ismaily ambao walikuwa wakipingana na maamuzi yake, wakati huo Club Africain ikiwa mbele kwa mabao 2-1.

Baada ya vurugu hizo kushamiri, mwamuzi wa kati aliamua kuuvunja mchezo huku mashabiki wakirusha chupa za maji na chupa za maji wachezaji Club Africain pamoja na maafisa wasimamizi wa mechi hiyo.

CAF pia imefuta matokeo yote ya Ismailia katika mechi za Kundi  C  na kundi hilo sasa linabaki na timu tatu ambazo ni CS Constantine ya Algeria, Club Africain na TP Mazembe ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC).

Ikumbukwe kuwa Yahya Zayd amejiunga na Ismailia mwezi huu akitokea Azam FC, akiungana na Himid Mao anayechezea klabu ya Ptrojet katika ligi ya nchi hiyo, ambaye alijiunga nayo mwanzon i mwa msimu huu.