
Mabigwa hao watetezi wa kupitia ukurasa wao wa Instagram wameweka video ikionyesha ukarabati ukiendelea katika uwanja huo.
Video hiyo inaonyesha ikisawazisha vifusi vilivyokuwa vimemwagwa uwajani hapo kwa siku kadhaa zilizopita.
Yanga imepanga kuukarabati uwanja huo wa kaunda na kuujenga uwanja huo pamoja na kujenga hosteli za kisasa za wachezaji.
Uwanja huo Kaunda maarufu (Jangwani) umekuwa ukiathiriwa mara kwa mara na mvua zinazonyeesha na kuusababishia kujaa maji.