Monday , 28th Jan , 2019

Kocha wa Simba, Patrick Aussems ameungana na kocha wa Yanga, Mwinyi Zahera, ambapo wote amesema makombe ya Mapinduzi Cup na SportPesa hayakuwa sehemu ya mipango yao.

Mwinyi Zahera na Patrick Aussems

Akiongea baada ya ushindi wa penalti 5-4 dhidi ya Mbao FC na kushika nafasi ya 3 kwenye michuano ya SportPesa, Aussems amesema ukweli ni kwamba ukishinda michuano hiyo safari yake inakuwa inaishia.

"Tunaitazama zaidi michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika ambapo tayari tumefikia lengo la kufika hatua ya makundi na bado tuna nafasi ya kufuzu robo fainali pia lengo kuu lingine ni kutetea ubingwa wetu wa Ligi Kuu Tanzania bara'', amesema.

Mapema kabla ya kuanza michuano ya Kombe la Mapinduzi kocha wa Yanga Mwinyi Zahera aliweka wazi kuwa haipo kwenye mipango yake na Yanga walipeleka kikosi cha pili na Zahera pia  hakwenda Zanzibar.

Makocha hao wawili wanatolea sana macho ubingwa wa ligi kuu ambao unaipa timu nafasi ya kuwakilisha nchi kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika mwakani.