Thursday , 21st Jan , 2016

Lleyton Hewitt amecheza mechi yake ya mwisho katika maisha yake ya mchezo wa tenesi,akipoteza kwa David Ferrer katika mashindano ya wazi ya Australia.

Lleyton Hewitt amecheza mechi yake ya mwisho katika maisha yake ya mchezo wa tenesi, akipoteza kwa David Ferrer katika mashindano ya wazi ya Australia.

Mchezaji huyo namba moja wa zamani,ambaye alishinda mataji mawili ya Grand Slam, alifungwa kwa 6-2 6-4 6-4.

"Sikuacha kitu kwenye chumba cha kubadilishia nguo. Nimejitolea kwa asilimia mia moja," alisema Hewitt raia wa Australia.

"Napenda kuja hapa na kushindana.Nimekuwa mwenye bahati kupata nafasi katika kipindi cha miaka 20 mfululizo.

Hewitt, aliyeshinda mataji 30 ya michuano mbalimbali, pia alitwaa mataji makubwa ya US Open mwaka 2001 na Wimbledon mwaka 2002, pia akiisaidia nchi yake kushinda kombe la Davis mara mbili mwaka 1999 na 2003.

Hewitt aliweka rekodi ya kuwa mchezaji mdogo kufuzu mashindano ya wazi ya Australia Januari mwaka 1997, mwezi mmoja kabla ya kutimiza umri wa miaka 16.

Pia aliweka rekodi ya kuwa mchezaji namba moja duniani mwenye umri mdogo aliposhinda nafasi hiyo mwaka 2001 akiwa na umri wa miaka 20 na miezi 9, akiivunja rekodi ya Mmarekani Ellsworth Vines, aliyekuwa mchezaji bora wa dunia akiwa na umri wa miaka 21, mwaka 1932.