Shujaa wa Barcelona kwenye mechi ya jana Luis Suarez ambaye alifunga mabao matatu peke yake katika mchezo huo.
Mabao yaliyoifanya Barcelona iibuke kidedea yalifungwa na wachezaji Lionel Messi ,Luis Suárez mabao aliyefunga matatu, Ivan Rakitic pamoja na Neymar Neymar da Silva Santos Júnior.
Ushindi huo mkubwa unaifanya Barcelona kuifuata Arsenal ikiwa kifua mbele kwenye mechi ya hatua ya 16 bora itakayopigwa wiki hii kwenye uwanja wa Emirate nchini Uingereza.
Mbali na mchezo huo michezo mingine Getafe iliambulia kichapo cha bao 1 – 0 kutoka kwa Atletico Madrid, Real Sociedad wao walichomoza na ushindi wa mabao 3 – 0 dhidi ya Granada CF, na Sevilla ikachapa bao 2 – 0 Las Palmas.
Kwa matokeo hayo Barcelona inaongoza ligi ikiwa na point 57, ikifuatiwa na Altetico Madrid kwa pointi 54, nafasi ya tatu ni Real Madrid yenye pointi 53, Villarreal ipo nafasi ya Nne na nafasi ya tano ni Sevilla ikiwa na point 40.