
Manchester United
Kauli hiyo inafuatia pigo la klabu hiyo baada ya kipa wake namba moja David De Gea kuumia goti wakati wa mazoezi na nafasi yake kuchukuliwa na kipa wa Argentina Sergio Romero.
Van Gaal amesema"Huwezi kufapata matokeo mazuri wakati nyota 13 wa kikosi cha kwanza ni majeruhi" hali inayompa wakati mgumu kupanga timu yenye kuleta ushindani.
Kuumia kwa De Gea kunamaanisha jitihada za klabu ya Manchester United za kuendelea kufanya vyema zinazidi mrama ambapo hivi karibuni nahodha wake Wayne Rooney aliumia goti kwenye mechi ya ligi kuu nchini Uingereza ambapo atakaa nje ya uwanja kwa wiki sita.
Mholanzi huyo amesema kikosi chake kilicheza vibaya dakika 15 za mwanzo na baadaye kikabadilika lakini akasisitiza sikuzote mambo yakienda kombo kila kitu kinachofuata kinaharibika.
Mashabiki wa klabu hiyo zaidi ya 800 walihudhuria mchezo huo uliopigwa nchini Denmark huku wakionekana kukerwa na matokeo ya klabu hiyo.