Tuesday , 11th Oct , 2016

Nyota wa Man United, Wayne Rooney, amesema ataendelea kuchezea timu ya Taifa ya Uingereza, licha ya kuondoshwa katika kikosi kitakachoanza hii leo, dhidi ya Slovenia, kutafuta tiketi ya kufuzu Kombe la Dunia 2018.

Wyne Rooney

Rooney, aliyecheza kwenye mchezo wa mwishoni mwa wiki iliyopita, na Uingereza kushinda 2-0 dhidi ya Malta, amesema kwa sasa ndiyo kwanza ana umri wa miaka 30 na angependa kucheza hadi akiwa na umri wa miaka 40, kama alivyokuwa winga wa Wales Ryan Giggs.

Rooney amekuwa akikosolewa kiwango chake, kushuka kadri siku zinavyokwenda, na hivi majuzi ameanza kuwekwa benchi, na kocha Jose Mourinho, kwenye kikosi cha Manchester United.

Nahodha huyo wa timu za Manchester United, na timu ya Taifa ya Uingereza, amefunga bao 1 pekee, kwenye michezo 12 kwa klabu yake pamoja na Timu ya Taifa, msimu huu.