Tuesday , 11th Oct , 2016

Msanii wa Bongo Fleva Rayvanny ambaye yupo katika lebo ya WCB amesema anamshukuru Mungun kutokana na namna mashabiki wanavyopokea kazi zake.

Rayvanny katika FNL ya EATV

Rayvanny ameyasema hayo alipokuwa katika kipindi cha Friday Night Live cha EATV akiwa na Diamond Platnumz kuelezea mafanikio ya ngoma yao ya ‘Salome’ pamoja na namna wanavyofanya kazi katika kampuni ya WCB.

“Ninamshukuru Mungu, ninapata sapoti kubwa kutoka kwa mashabiki na ninaahidi kuendelea kufanya mambo mazuri zaidi na ninawaomba wazidi kuniunga mkono” Amesema Rayvanny.

Kuhusu ngoma ya Salome, Diamond amesema Rayvanny alipopewa ajaribu kuingiza sauti alionekana kuitendea haki zaidi, na ndiyo maana akaamua afanye naye ngoma hiyo badala ya mtu mwingine kutoka katika kampuni yao ya WCB.