
Msemaji wa ofisi ya haki za binadamu ya Umoja wa Mataifa Cecile Pouily.
Ofisi hiyo imesema hatua hiyo imefikiwa baada ya serikali ya Burundi baada ya kuamua kutotoa ushirikiano tena.
Akizungumzia hatua hiyo msemaji wa ofisi hiyo Cecile Pouily amesema wanatiwa wasiwasi na uamuzi wa serikali ya Burundi kuamua kusitisha ushirikiano wa aina yoyote na ofisi yao
Ameongeza kuwa ingawa ofisi hiyo imejitahidi na kufanikisha masuala mengi lakini sasa ni mapema kujua mustakhbali wao Burundi kwa kuwa nchi hiyo hivi sasa iko katika wakati muhimu sana , na ni muhimu majadiliano kuhusu hali ya haki za binadamu yakaendelea.