Thursday , 13th Oct , 2016

Hatua ya serikali ya Kenya kukimbilia kusafirisha mafuta ghafi katikati ya uchaguzi mkuu mwakani itaigharimu taifa hilo hasara ya shilingi bilioni 4 za nchi hiyo, ripoti ya asasi moja ya kiraia nchini humo imesema.

Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta.

Asasi hiyo ya Jukwaa la Jamii ya Kenya kuhusiana na rasilimali za Mafuta na Gesi, imesema katika ripoti yake hiyo kuwa mpango huo unazua maswali mengi ikizingatiwa hali ya bei ya mafuta ghafi ya sasa katika soko la dunia.

Ripoti ya ripoti hiyo iliyotolewa jana imesema kusafirisha mafuta ghafi kwa barabara kwa umbali wa kilomita 800 ni gharama kubwa na kutachangia kupatikana kwa hasara kubwa, ambayo ingeweza kuokolewa kwa kujengwa miundombinu stahiki kama bomba la mafuta.