Thursday , 13th Oct , 2016

Uchumi wa Chad unapoteza jumla ya 'Chad Franc' bilioni 575.8 sawa na dola za Marekani billion 1.2 kwa mwaka au asilimia 9.5 ya pato la taifa kutokana na athari za lishe duni kwa watoto, imesema ripoti ya utafiti mpya iliozinduliwa mjini Djamena.

Watoto wakimbizi nchini Chad

Ripoti hiyo iliyopewa jina la "Gharama za njaa barani Afrika: inaonesha kwamba fedha nyingi zinapotea kutokana na ongezeko la gharama za huduma za afya, mzigo zaidi wa mfumo wa elimu na uzalishaji mdogo wa wafanyakazi.

Utafiti unaonesha kwamba asilimia 56.4 ya watu wazima walikabiliwa na maradhi ya kudumaa walipokuwa watoto, na hii inawakilisha zaidi ya watu milioni 3.4 ya nguvu kazi ya taifa hilo ambayo haiwezi kufikia kilele cha uwezo wao wa kufanya kazi kutokana na athari za lishe duni utotoni.

Uwezo mdogo wa kimwili katika uzalishaji unalipotezea taifa la Chad Franc bilioni 63.7 kwa mwaka kutokana na maradhi yenye uhusiano na lishe dunia ya utotoni , huku maradhi hayo yakigharimu Franc zingine bilioni 168.5 kwa matibabu.