
Alhaj Ali Hassan Mwinyi
Alhaj Mwinyi ametoa hotuba ya ufunguzi ya mafundisho kwa viongozi wa sasa na wa baadaye yaliyofanyika jijini Dar es Salaam ambapo ameongeza kuwa miaka 17 ya kifo cha baba wa taifa ni fursa ya kujitathmini.
Mzee Mwinyi ameeleza kuwa kwa sasa ni wakati wa kutafakari nini kimesababisha mpaka nchi ikawa haina uadilifu alioujenga Mwalimu Julias Kambarage Nyerere wakati wa uongozi wake.
Amesema kuwa nafasi ya mdahalo huo inawapasa viongozi hao kukaa kutafakari namna ya kurudisha nchi kwenye reli ambayo iliachwa na mwalimu Nyerere ambaye ndiye muasisi wa taifa hili katika misingi ya uongozi.
Akizingumza katika Mdahalo huo Mtendaji Mkuu wa Taasisi ya Mwalimu Nyerere Joseph Butiku, amesema ni vyema ukawepo usawa kwa watu wote na watu wanaoheshimu misingi ya uongozi.