
Dhahiri Kidavashari
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya Dhahiri Kidavashari amesema kuwa ajali hiyo imetokea mnamo tarehe 18.10.2016 majira ya saa 9:50 Alasiri ikihusisha gari lenye namba za usajili T.841 BRW aina ya Isuzu basi likitokea Wilaya ya Chunya kwenda Mbeya.
Amesema gari hilo lililokuwa likiendeshwa likiendeshwa na dereva aitwaye ELIA ISACK [37] Mkazi wa Chunya liliacha njia, kupinduka na kusababisha vifo kwa abiria wanne ambao ni HAWA MOHAMED [30] mkazi wa Chunya, Mtoto mdogo wa miaka 2 wa kiume ambaye bado kufahamika jina lake na wanaume wawili ambao hawakufahamika majina yao.
Amesema chanzo cha ajali hiyo ni mwendo kasi na kwamba majeruhi wote wamelazwa Hospitali ya Rufaa Mbeya na dereva amekamatwa huku upelelezi ukiwa bado unaendelea.
Aidha katika ajali abiria 22 walijeruhiwa kati yao wanawake 14 na wanaume 08.
Katika matukio mengine, mnamo tarehe 18.10.2016 majira saa 3:41 usiku huko eneo la Mlima Nyoka, Kata ya Itewe, Tarafa ya Tembela, Wilaya ya Mbeya Vijijini, Gari lenye namba za usajili T.660 APR aina ya Toyota Pick up ikiendeshwa na dereva aliyefahamika kwa jina la JACOB SANGA iliacha njia na kupinduka kisha kusababisha kifo cha RAHEL SASITA [55] Mkazi wa Itewe na watu wawili kujeruhiwa.
Aidha mnamo tarehe 18.10.2016 majira ya saa 2:50 usiku huko katika Kijiji na kata ya Itope, Tarafa ya Unyakyusa, Wilaya ya Kyela, Mkoa wa Mbeya, Gari lenye namba za usajili T.574 BNQ aina ya Toyota Coaster mali ya Kanisa la Uinjilisti Kiwira ikiendeshwa na dereva JAFARI SIMON [27] mkazi wa Tukuyu ilimgonga mpanda baiskeli aliyefahamika kwa jina la WEMA EDWIN [10] mwanafunzi wa darasa la tano katika Shule ya Msingi Mbogola na kusababisha kifo chake papo hapo.
Chanzo cha ajali ni mwendo kasi. Dereva amekamatwa. Upelelezi unaendelea.