
Mkuu wa wilaya ya Arumeru, Alexander Mnyeti.
Hayo wamebainika katika ziara ya kushtukiza iliyofanywa na Mkuu wa Wilaya ya Arumeru, Alexander Mnyeti, ambapo pia amebaini ushiriki mkubwa wa viongozi wa serikali katika kilimo hicho, hivyo kufanya jitiahada za serikali katika kukomesha kilimo hicho kusuasua.
Katika kudhibitisha hilo baadhi ya watendaji wa kata ya Lemanyata walianza kuyakana maeno yao kwa madai kuwa wahawezi kushiriki katika kukomesha bangi katika maeneo yaliyo nje ya mipaka yao.
Maelezo hayo ndiyo yalimlazimu mkuu huyo wa wilaya kumuagiza OCD wa Arumeru, kuwakamata viongozi wote wa serikali ya kata akianzia kwa diwani wa kata hadi wenyeviti wa vitongoji.
Vijiji vilivyotembelewa ni Lenjani na Lemanyata, ambapo muda mfupi baadaye imeshuhudiwa mashamba yakiwa yamefyekwa bhangi na kuanza kuchomwa, jambo lilomlazimu mkuu wa wilaya kushuka na kubeba masalia kama ushahidi.