Akipiga stori kwenye Planet Bongo ya East Africa radio, Jay Moe alisema watu wametafsiri vibaya kwa kumuhusisha Izzo na wimbo huo pia kumuweka kwenye kundi la wasiojua ni kosa , na kuongeza kuwa yeye amewachana watu wote ambao wanafanya kazi mbaya na kusumbua watu kuwasaidia kuweka picha za kazi zao katika mitandao ya kijamii.
“Mimi sina bifu na Izzo Biznezz, siwezi kumtungia nyimbo za kumchana. Mimi sijamlenga mtu mmoja kwenye wimbo wangu bali nimewachana wote wanaoandika nyimbo mbovu sana alafu anakutumia umsaidie kuweka kwenye mitandao hata mwezi mzima alafu wimbo ukija kuusikia unatamani kufuta picha" Alisema Moe.
Majibu hayo yamekuja baada ya tetesi zilizopo mitaani ya kwamba katika wasanii wanaoongoza kwa kuomba watu waweke matangazo ya nyimbo zake kwenye mitandao lakini akitoa nyimbo zinabuma kwa kuwa hawekezi kwenye kuangalia kuandika nyimbo bali picha.