Winga huyo aliwaweka kwenye wasi wasi maafisa wa Shirikisho la Soka Afrika (CAF) baada ya kuonesha kiwango kikubwa cha uchezaji huku akiwa na pumzi za hali ya juu na kusababisha timu yake kuibuka na ushindi wa bao 2-1.
Kitendo hicho kilisababisha kupelekwa katika vipimo mara baada ya kipenga cha mwisho kupulizwa na kusababisha kushindwa kuenda kupokea tuzo yake ya mchezaji bora 'Man of the match' na matokeo yake ikabidi awakilishwe na mlinzi Dickson Job