Monday , 5th Jun , 2017

Ushindi wa Golden State Warriors wa vikapu 132 -113 dhidi ya Cleverland Cavaries umeweza kuwaweka katika nafasi nzuri baada ya kuwagaragaza wapinzani wao alfajiri ya kuamkia leo katika uwanja wa Oracle Arena, Oakland nchini Marekani.

Mchezaji Kevin Durant akiingiza mpira kweye kikapu

Kutokana ushindi huo Warriors wanazidi kung'ara baada ya kuwapiga wapinzani wao Cavs mara mbili mfululizo katika fainali za NBA huku mchezaji Stephen Curry na Kevin Durant wakijiwekea rekodi mpya katika michuano ya kuwa wachezaji wa kwanza kutoka timu moja kufikisha usawa wa alama zaidi ya 30 katika mechi mbili za mwanzo za fainali za NBA.

Ushindi huo wa Warriors umeweza kurudisha tabasamu la kocha wao Steve Kerr ambaye amerejea katika timu kwa mara ya kwanza tangu Aprili 19 kutokana na kusumbuliwa na maradhi.

Kocha mkuu wa Warriors Steve Kerr akibadalishana mawazo na mchezaji Stephen Curry