Wednesday , 20th Dec , 2017

Wasanii wa muziki wa kizazi kipya Sogy Dogy na Ben Pol, wamekishukuru kipindi cha Planet Bongo kinachorushwa na East Africa Radio, kwa kuonyesha uzalendo na kusapoti muziki wa wasanii wa nyumbani.

Wakizungumza kwenye kipindi hiko msanii Sogyy Dogy ambaye ni mkongwe kwenye sanaa ya muziki wa bongo fleva nchini, amesema kitendo hicho kinawapa faraja wasanii wa bongo.

Kwa kweli kwa mwaka huu nitoe pongezi kwa Planet Bongo na East Africa Radio kiujumla kwa yale masaa matatu ya bongo fleva, unajua ukiangalia kwenye chati nyimbo 10 zilizopigwa sana kwa mwaka 2016 kulikuwa kuna ngoma 3 za wanaigeria tena zikiwa kwenye nafasi ya juu, na nina uhakika mwaka huu, kinakuja kutokea tena, sasa nenda Kongo nenda huko Nigeria, 10 bora huwezi kukuta ngoma ya bongo, tujifunze kitu kwa hili”, amesema Soggy Dogy.

Naye Ben Pol aliongeza kwa kusema kwamba watanzania tunatakiwatuone aibu kwa hili na kujisikia vibaya pale tunapoacha kusapoti muziki wa nyumbani na kuendekeza wa nje.

Inatakiwa ifike hatua uone kwamba kushindwa kumsapoti msanii wa nyumbani kwangu ni ushamba, unatakiwa ujisikie hivyo”,amesema Ben Pol.

Kipindi cha Planet Bongo kinachorushwa na East Africa Radio, kina masaa matatu ambayo kinapiga muziki wa bongo fleva peke yake, huku ndani ya masaa hayo, saa moja unapigwa muziki wa hip hop ya Tanzania peke yake na kuwa kipindi pekee kinachosapoti muziki wa Tanzania kwa asilimia mia.