
Martha ameyasema hayo kwenye kipindi cha Kikaangoni kinachoruka kupitia Ukurasa wa East Africa Television kwenye mtandao wa 'Facebook' ambapo pamoja na kukataa kumbania amekiri kuwa Beatrice ana uwezo mkubwa kuliko yeye.
''Unajua kuna vitu vingine hata ukibana unaonekana mjinga, mimi ndio chanzo cha Beatrice kuimba najua hilo, sio kwamba namwandikia lakini ana uwezo mkubwa kuliko mimi kwahiyo siamini kama naweza kumbania'', alisema.
Martha ameongeza kuwa hizo tetesi hawezi kuzikwepa kwasababu watu wakishatokea familia moja na wanafanya kitu kinachofanana lazima watu watatafuta chokochoko.
Aidha Martha ameweka wazi kuwa yeye na mdogo wake wapo vizuri tangu anaanza hadi sasa ndio mana walifanya nyimbo za pamoja lakini kikubwa ni ratiba zao kuna muda huwa zinapishana ndio maana hawafanyi nyimbo nyingi za pamoja.