Monday , 26th Nov , 2018

Serikali imewaagiza wananchi wote wa Mitaa ya Kasanga na Mindu wa Wale Wanaoishi Ndani Ya eneo la hifadhi ya bwawa la Mindu manispaa ya Morogoro kuondoka Kwa hiyari hadi kufikia januari 31 mwakani ili kupisha upanuzi bwawa la mindu

Wananchi wakiwa kwenye mkutano, bwawa la maji.

Agizo hilo la kuondolewa wananchi hao limetolewa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Maji Prof, Kitila Mkumbo kufuatia mgogoro mkubwa uliokuwa ukiendelea baadhi ya wananchi wa mitaa ya kata ya mindu na bodi ya maji bonde la wami ruvu juu ya uvunjwaji wa sheria ya matumizi ya maji inayokataza kufanyia shughuli yeyote ya kibinadamu mita 500 kutoka katika chanzo cha maji

Profesa Mkumbo amebainisha kuwa baada ya  kupitia nyaraka mbalimbali na kukagua mipaka ya bwawa la Mindu, serikali imejiridhisha kuwa uwepo wa shughuli za kibinadamu ndani ya hifadhi ya bwawa hilo kunahatarisha uhai wa bwawa pamoja na wananchi wenyewe.

Tamko hilo la serikali limeonekana kuwa mwiba kwa wananchi hao na kujikuta katika hali ya huzuni ambapo wanachi hao wameiambia www.eatv.tv kuwa sheria iliyopo kwa sasa imekuwa ni shubiri kwao hivyo wanaiomba serikali kupunguza eneo la uhifadhi kuoka mita 500 hadi kufikia mita 400.