Thursday , 29th Nov , 2018

Mbunge wa Vunjo kupitia NCCR-Mageuzi, James Matia amedai aliwemnda kuonana na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa ajili ya kumueleza malalamiko yake juu ya Mkuu wa Wilaya ya Moshi, Kippi Warioba kwa madai ya kusitisha ujenzi wa barabara na kupelekea hasara ya mabilioni.

Mbunge wa Vunjo James Mbatia na Rais Dkt, John Pombe Magufuli

Mbatia ametoa kauli hiyo wakati akizungumza na wananchi wa Jimbo lake kata ya Makuyuni katika mamlaka ya mji mdogo wa Himo, wilaya ya Moshi wakati wa Mkutano wa hadhara baina ya kiongozi huyo na wananchi.

Nilibahatika hivi karibuni, Rais Magufuli aliniita akasema, ameshaagiza vyombo vyake na wengine wameniita Dodoma, barabara za wana Vunjo atachangia yeye binafsi kama John Pombe Magufuli, pili serikali yake itachangia na tatu atakuja kama Amiri Jeshi Mkuu kufungua barabara hizi yeye mwenyewe," amesema Mbatia.

Mbatia ameongeza kuwa: “sasa tuone ni nani zaidi ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na maendeleo ya watanzania, maendeleo hayana itikadi za vyama. Kwa nini amefanya hivyo, kwa sababu Jimbo la Vunjo tumekuwa wa kwanza Tanzania kuweza kujipanga wenyewe mpaka hatua tuliyofikia ya kujiletea maendeleo yetu wenyewe.”

Mradi wa upanuzi na ujenzi barabara za vijijini kwa kiwango cha changarawe unaodaiwa kusisitishwa katika Jimbo la Vunjo mkoani Kilimanjaro, unahusisha barabara zenye urefu wa kilometa 389.3 ambazo zilikuwa zigharimu Sh. bilioni 12.077 kutokana na utafiti wa Wakala wa Barabara za Vijijini na Mijini(Tarura).

Novemba 15 mwaka huu kupitia wakili wa kujitegemea, Harlod Sungusia alizungumza na waandishi wa habari juu ya madai ya kumshtaki Mkuu wa Wilaya ya Moshi, Kippi Warioba kwa madai ya kudaiwa fidia ya zaidi bilioni 2.