
Kikosi cha Yanga na mlinda mlango mwenye jezi nyeusi ni Klaus Kindoki
Kupitia taarifa yake, Yanga imempa pole mchezaji huyo ambaye amejiunga na timu mismu huu wa 2018/19 na tayari ameshacheza mechi kadhaa za ligi kuu soka Tanzania bara.
''Uongozi wa Yanga unatoa pole kwa mchezaji Klaus Kindoki pamoja na familia yake kwa kumpoteza Baba yake. Msiba upo kwao Congo DRC na mazishi yatafanyika siku ya Jumapili uko uko kwao Congo'', imeeleza taarifa ya klabu.
Kindoki alikuwa langoni kwenye mchezo wa ligi kuu kati ya timu yake ya Yanga dhidi ya Mwadui FC ambapo vinara hao wa ligi waliibuka na ushindi wa mabao 3-1 na kuzidi kujikita kileleni wakiwa na alama 53.