
Makonda ameandika "shukrani kwake muumba wa mbingu na ardhi kwa kumpa kaka yetu Tundu Lissu afya na siha njema''.
"Wengi walioko jimboni Singida na watanzania wote walihangaika kwa sala na maombi, usiku na mchana, wengine wakichanga pesa zao na hatimaye mola akajibu maombi yao." ameandika Makonda.
"Kwa heshima na kuonyesha uzalendo, nakushauri Kaka yangu Tundu Lissu rudi nyumbani utoe shukrani zako kwao. Watu wako wamekumiss zaidi ya hao unaowakimbilia hivi sasa."
"Ziara yako huko haina tija kwa yoyote, na kuichafua Serikali si kumchafua Mh. Rais ni kuichafua Tanzania yetu sote na wewe ukiwemo."