
Akizungumzia katika kipindi cha maswali na majibu Bungeni jijini Dodoma, Mbunge Kessy ameeleza mama huyo kwa sasa hali yake ni mbaya zaidi, lakini alifanikiwa kujifungua na mtoto wake anaendelea vizuri.
Mbunge Kessy amesema kuwa "vifo vingine vya kinamama vinatokana na kina mama wenyewe, juzi tu jimboni kwangu kuna mama mmoja tena zao lake la nane, kachelewa mwenyewe makusudi kwenda kituo cha afya"
"Yule mama akaamua kujifanyia oparesheni mwenyewe kwa kutumia wembe na katoa mtoto, sasa hivi yuko Hospitali hali yake si nzuri ila hali ya mtoto ni nzuri, kwa hiyo wakati mwingine vifo vya kina mama vinatokana na wao wenyewe" amesema Mbunge Kessy.