''Nafasi ya kiti hiki cha usemaji wa @SimbaSCTanzania sitakikalia miaka yote lazima kuna siku nitakiachia na sio mimi tu NI kwa yeyote hata baada ya mimi, kwasasa ibaki hivyo kiti hiki nakikalia mimi'' - @HajiManara #SimbaPress pic.twitter.com/hUTbyZ7yS7
— East Africa TV (@eastafricatv) August 20, 2019
Akiongea leo na wanahabari, Manara amesema kuwa mara nyingi vitu vingi vinaanzishwa mitandaoni na sio lazima yeye avitolee ufafanuzi lakini suala la kufukuzwa hajafukuzwa, japo ukweli ni kwamba hatokaa kwenye nafasi hiyo milele.
Aidha Manara amewataka mashabiki wa Simba kujitokeza kwa wingi uwanjani siku ya Jumapili kwenye mchezo wao wa marejeano dhidi ya UD Songo ya Msumbiji, utakaopigwa kwenye uwanja wa taifa.
''Nawaomba wanasimba na watanzania wote, waje uwanjani siku ya Jumapili na tiketi tutaanza kuuza mapema sana siku ya Alhamis na mimi kwenye Champions League huwa napenda kukaa kwa mashabiki'' - @HajiManara #SimbaPress pic.twitter.com/gaNve2E4bm
— East Africa TV (@eastafricatv) August 20, 2019
Zaidi tazama Video hapo chini