
TAKUKURU
Mtuhumiwa huyo ambaye ni Katibu wa Msikiti wa Nyakato Rahman amekuwa akiwapigia simu baadhi ya viongozi mbalimbali wa serikali na wanachi kwa kuwaambia kuwa wanatuhuma na kuwataka kufika ofisni kwakwe kwa ajili ya mahojiano na kuwaomba fedha kwa ajili ya kuwasaidia.
Akizungumza na wanahabari ofisini kwake, Kamanda wa TAKUKURU mkoa wa Mara, Alex Kuhanda amesema mtuhumiwa huyo amekamatwa na simu tano pamoja na laini saba mitandao mitatu tofauti.
Aidha Kamanda amesema ofisi yake inautararibu wa kumwita mtuhumiwa na kufanya nae mahojiano ya ana kwa ana na sio kufanya maojiano kwa njia ya simu ama ujumbe mfupi, hivyo anawataadharisha wananchi kuwa makini na matapeli wa namna hiyo.
Uchunguzi unaendelea na utakapokamilika, mtuhumiwa huyo atafikishwa mahakami kwa ajili ya hatua zaidi za kisheria.