Mbwana Samatta akiwa TP Mazembe
Samatta ametumia ukura wake wa Twitter kuhoji hivyo akieleza kuwa haelewi tatizo liko wapi maana wachezaji wa Tanzania ambao wanacheza TP Mazembe hawazingatiwi.
''Ni TP mazembe imepungua ukubwa au wachezaji wetu wa kitanzania waliopo pale ndo sio wakubwa? naona kama hatuna habari nao ivi'', ameindika Samatta.
Ni tp mazembe imepungua ukubwa au wachezaji wetu wa kitanzania waliopo pale ndo sio wakubwa? naona kama hatuna habari nao ivi.
— Mbwana Samatta (@Samagoal77_) November 25, 2019
Wachezaji wa Tanzania wanaocheza TP Mazembe kwasasa ni Eliud Ambokile pamoja na Ramadhan Singano.
Akiwa TP Mazembe kwa takribani miaka mitano, Samatta alifanikiwa kuwa mshambuliaji hatari Afrika huku akiibuka mfungaji bora wa Ligi ya Mabingwa Afrika na kutwaa tuzo ya mchezaji bora wa ligi za ndani Afrika mwaka 2016.
Ramadhani Singano (kushoto) na Eliud Abokile (kulia)