Friday , 13th Dec , 2019

Mfalme wa BongoFleva Ali Kiba, amemtaja msanii Nay wa Mitego, kama shabiki yake namba moja kwenye upande wa kuangalia picha na video anazoweka kwenye mtandao wa Whatsapp.

Wasanii wa Muziki Bongo, Ali Kiba na Nay wa Mitego.

Ali Kiba amesema hilo kwenye Planet Bongo ya East Africa Radio, wakati anatambulisha wimbo mpya wa msanii wake Killy kutoka kundi la Kings Music, uitwao Gubu, ambapo aliulizwa kuhusu uwezekano wa Nay wa Mitego kuwepo kwenye tour yake ya AliKibaUnforgettable Tour kwa Mkoa unaofuata.

"Kwa bahati nzuri Nay huwa nachati naye kila wakati, yaani katika mashabiki zangu wanaopenda  kuangalia status yeye namba moja, huwa tunawasiliana sana akipata nafasi huwa ananicheki na vilevile tumelizungumza hilo suala, lakini ratiba zake kidogo zimebana kwenye safari ya Iringa, ila safari ijayo atatia mguu" ameeleza Ali Kiba.

  Aidha Ali Kiba ametangaza Mkoa wa Iringa, kama ndiyo utafuata kwenye kufanya ziara yake ya kimuziki na kwamba safari hii msanii Christian Bella ni miongoni mwa wasanii watakaoenda kushambulia jukwaa mkoani humo