
Ugonjwa wa Akili
Takwimu hizo zimetolewa leo jijini Dodoma na Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali hiyo Dkt Erasmus Mndeme, katika muendelezo wa ukaguzi wa huduma za afya zinazotolewa katika Mkoa wa Dodoma.
Dkt, Mndeme amesema kuwa tatizo hilo limeongezeka, kutokana na matumizi ya dawa za kulevya wakati asilimia 75 ya wagonjwa wa akili ni wanaume, huku wanawake wakiwa ni asilimia 25 na asilimia 99 ya wagonjwa wa akili hutibiwa na kuondoka.
Aidha Dkt. Mndeme amesema mpaka sasa Hospitali hiyo ina jumla ya wagonjwa 450, ambao wamelazwa kutokana na hatua ya ugonjwa ulipofikia kuhitaji uangalizi maalum.